Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia: Wabunge acheni ubabe migodini
Habari za Siasa

Rais Samia: Wabunge acheni ubabe migodini

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia amewaonya wabunge kuacha kufanya ubabe katika maeneo ya migodi ili wapewe pesa na kuzitumbua badala yake wasimamie pesa hizo za hisani zitumike kwa maendeleo ya Taifa na wananchi kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amewaasa wawekezaji katika miradi ya uchimbaji wa madini kuzingatia kwamba suala la kurejesha fadhila kwa wananchi sio la hiyari.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Disemba, 2021 katika hafla ya utiaji saini mikataba baina ya serikali na kampuni za uchimbaji madini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza mali hiyo imeumbwa pale walipo hivyo ni mali yao wao na serikali.

“Kama tunakwenda kuichukua, kuichimba, kuitengeneza… lazima turudishe fadhila kwao wafaidike na kile Mungu alichowaumbia, sio tuende kuchota tuondoke, tuwaache walivyo. Kwa suala la fadhila halina hiyari,” amesema.

Pia amewaomba waakuu wa wilaya, wabunge wa maeneo husika na serikali za mitaa kutoa ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa miradi hiyo.

“Sio kwenda kufanya ubabe migodini, kuchukua fedha ya hisani kwa wananchi na ikatumika kwa mambo mengine.

“Wabunge ambao maeneo yenu miradi hii ipo, miradi inakuja kwenu iwasaidie kujenga maendeleo ya nchi si kujijenga ninyi binafsi… kuna ile kwenda na kuwatisha wenye migodi huko kwamba kama si mimi ninyi msingekuwa hapo. Hapana!!

Amesema iwapo faida ya miradi hiyo ikirudi kwa wananchi ni alama ya kipekee kwa mbunge husika kwamba amehusika kuwa sehemu ya ujio wa mradi huo.

Aidha, ameongeza kuwa moto wa madini ulianza kuwashwa na Rais Dk. John Magufuli na yeye atauendeleza na hautazimika ili wananchi wanufaike.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!