Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB bonge la mpango yamwaga zawadi milioni 23
Habari Mchanganyiko

NMB bonge la mpango yamwaga zawadi milioni 23

Spread the love

 

BENKI ya NMB katika kipindi cha wiki tisa, imetumia Sh.117 milioni katika kampeni ya weka akiba na ushinde inayoitwa ‘NMB Bonge la Mpango 2.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika kipindi cha wiki mbili za kampeni hiyo, NMB imemwaga zawadi zenye thamani ya Sh.23.5 milioni kwa mpigo.

Droo mbili kwa mpigo za ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ zimefanyika Jumatano jijini Dar es Salaam, ikiwamo ya mwisho wa mwezi (Novemba) iliyotoa zawadi za pikipiki tatu za mizigo aina ya Skymark na droo ya wiki ya tisa iliyotoa washindi 12, kati ya hao 10 wakishinda fedha taslimu na wawili wakijinyakulia pikipiki hizo miguu mitatu.

Katika droo hiyo iliyofanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Saleh Omari (wa Tawi la Chakechake), Kelvin Masava (Mwenge) na George Nyaisonga (Mbalizi Road), walitangazwa washindi wa mwisho wa mwezi Novemba wa pikipiki za mizigo zenye thamani ya Sh.4.5 milioni kila moja.

Nao Ludovick Damas (Masasi) na Ally Mnyone (Tawi la Madaraka), waliibuka washindi wa pikipiki mbili za droo ya tisa, iliyotoa pia washindi 10 wa fedha taslimu, wakiwemo Luqman Khamis (Congo Street), Wilfred Rajabu (Mlimani City) na Alberth Fanuely (Madaraka).

Washindi wengine wa pesa taslimu waliopatikana katika droo ya tisa ni pamoja na Ramadhani Maambe (Chalinze), Upendo Israel (Kahama), Rashid Mussa (Lindi), Melkiory Mholya (Songea), Victoria Bunyinyiga (Tarime), Msafiri Daffa (Wami) na Meshack Jonathan (SM-Kenyatta Road).

Aidha, pikipiki tano za mizigo zilizotolewa wiki hii, zinafanya kampeni hiyo hadi sasa kuwa imeshatoa jumla ya pikipiki 24 zenye thamani ya Sh.108 milioni, kati ya pikipiki 50 zitakazotolewa katika kampeni yote, ambako zawadi za pesa taslimu zimefikia Sh.9 milioni, hivyo thamani ya jumla ya zawadi zote kufikia Sh. Mil. 117.

Kwa Sasa NMB Bonge la Mpango imebakisha pikipiki 26 zenye thamani ya Sh.117 zinazoshindaniwa, sambamba na pesa taslimu Sh.3 milioni zitakazoenda kwa washindi 30 wa wiki tatu zilizobaki kuhitimisha kampeni hiyo ambayo ina zawadi zenye thamani ya Sh.237 milioni.

1 Comment

  • Alisikika AKISEMA:-

    NIPE KIWANJA – (HALIMASHAURI YA TEMEKE IKAMPA BURE)

    NIJENGEE KWANGU – (NHC IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA MAJI – (MAMLAKA YA MAJI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA UMEME – (TANESCO IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA SYSTEM YA MAJI MACHAFU – (MAMLAKA YA MAJI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA BARABARA – (TANROAD IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA GOBOLE – (WIZARA YA ULINZI IKAFANYA KAZI)

    NYUMBANI KWANGU LETA MWANAMKE – (KAMPUNI YA WANAMWAKE IKAFANYA KAZI)

    KWELI ALIKUWA MWANAJESHI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!