Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jenerali Mabeyo:Vita ya ugaidi ngumu
Habari MchanganyikoTangulizi

Jenerali Mabeyo:Vita ya ugaidi ngumu

Spread the love

 

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, amewaomba wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama katika kukabiliana na ugaidi kwa kuwa vita hiyo ni ngumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 27 Novemba 2021, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio na changamoto za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ndani ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, amesema vita hiyo ni ngumu kutokana na mbinu zinazotumiwa na magaidi kuwa si rahisi kuwatambua kutokana na kujigawa katika vikundi vidogo vidogo.

“Vita hii ni ngumu, inahitaji umakini mkubwa kwa sababu mbinu wanazotumia katika mapigano hayo sio ule utamaduni wa mapigano ya kawaida, wanapigana katika vikundi vidogo vidogo,” amesema Jenerali Mabeyo.

Jenerali Mabeyo amesema, viashiria vya ugaidi vipo huku akikumbushia tukio la mauaji ya wananchi katika wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.

“Tunayo matishio mengi kutoka nje lakini tunayo ndani, viashiria vya ugaidi vipo. Vilevile nchini kwetu na hivi naamini nyie ni walewa wakubwa, ni vita ambayo imeanzia mataifa mengine na inasogea, imekuja mpaka kwetu,” amesema Jenereli Mabeyo.

Jenerali Mabeyo amesema “kama mnakumbuka ilianzia mbali, tuliona mkoani Tanga maeneo ya Amboni, wakateremka wakaja Kibiti, kama mtakumbuka maeneo ya Kibiti, Mkuranga tulipambana kidogo na wakateremka Kusini tukapambana nao kule Mtwara na Ruvuma wakavuka mipaka wengine ndiyo sasa unawasikia wako Msumbiji.”

Jenerali Mabeyo amesema, kazi wanayoifanya sasa ni kuhakikisha wanadhibiti hali hiyo kwa kushirikiana na wananchi.

“Lakini kazi kubwa inayofanyika kuhakikisha tunadhibiti hali hiyo na msaada mkubwa lazima utoke kwa wananchi, ndiyo wanaoishi na vikundi hivi. Wako miongoni mwetu bila kufichuliwa na wananachi JWTZ haiwezi kukabiliana nao,” amesema Jenerali Mabeyo na kuongeza:

Jenerali Mabeyo amesema “ulinzi ni wa Watanzania wote, kila mahali ulipo matukio unayaona vishirikishe vyombo vya ulinzi na usalama ili viweze kukabiliana nao hasa mbinu wanazotumia mara nyingine wanastukiza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!