Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Mkuu atoa maagizo mazito sekta ya misitu
Habari Mchanganyiko

Waziri Mkuu atoa maagizo mazito sekta ya misitu

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) kuendelea kuwawezesha wajasiriamali wanaowekeza kwenye misitu kwa kuwapatia ruzuku itakayowezesha kunufaika na rasilimali ya misitu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa …  (endelea).

Pia ameuagiza mfuko huo kufungua tawi katika mkoa wa Iringa ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa mazao ya misitu kupata huduma kwa urahisi.

Majaliwa ametoa maagizo hayo leo tarehe 13 Novemba, 2021 wakati akifungua kongamano la uwekezaji wa sekta ya misitu Mkoa wa Iringa.

Ameiagiza wizara ya maliasili nna utalii kuhakikisha wawekezaji wanaendeleza mkakati wa kuwanuisha wananchi wanaoishi jirani na misitu kupitia miradi ya ufugaji nyuki.

Amesema wizara hiyo inatakiwa kuweka mazingira wezeshi ili misitu izalishe ajira nyingi. Wizara ya maliasili wanaweza kuzungumza na Tamisemi kuona namna ya kuongoza wananchi kunufaika na rasilimali hii.

Pamoja na mambo mengine ameuagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali ya misitu kwenye mashamba ya miti, hifadhi ya misitu, mapori ya akiba, mapori tengefu na wananchi washirikishwe kwenye maeneo hayo ili waweze kunufaika.

“TFS ishirikiane na Mamlaka nyingine ikiwemo TAWA, halmashauri kuendelea na utatuzi wa migogoro baina ya wananchi wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa kuhakiki mipaka na vigingi vingine vinavyoonekana.

“Wizara hakikisheni sera, sheria, kanuni na miongozo kwa ajili ya kusimamia rasilimali za misitu na nyuki zinafanyiwa mapitio ya mara kwa mara ili kukidhi mazingira ya sasa ya uwekezaji hasa kukidhi matakwa ya mkuu kiongozi wa nchi aanataka wananchi wafaidike na misitu.

“Wizara hakikishe mamlaka zote zinakuwa imara zina watumishi na watendaji wa kutosha ili zinashiriki kikamilifu kwa kupita kwa wananchi na kutoa elimu. Pia taasisi hizo zitoe tahadhari ya mambo hatarishi pale wanapokwenda tofauti kwani ukataji miti bila kupanda miti haukubaliki,” amesema.

Aidha, ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha haraka taratibu zinazonzisha

mamlaka ya misitu ili kusimamia kikamilifu kuboresha na kuongeza uzalishaji wa mazao ya misitu hapa nchini.

“Harakisheni kutafuta masoko, tujitahidi kujua masoko yako wapi, pia kaeni na wawekezaji wetu wanajua masoko yako wapi. Tufike mahali badala ya mtu kutupelekea sisi tupeleke hukohuko.

“Wizara iendelee kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uanzishwaji wa viwanda, tunakata kuwa na viwanda vingi vya kuchataka misitu. Hatuna sababu ya kuagiza kama vile kuagiza nguzo.

“Tuendeleze program za upandaji miti, na kutunza mazingira na kuongeza kipato kwa wananchi na taifa na kuongeza hewa ya ukaa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!