WIZARA ya Habari Mawasiliano na Teknologia ya Habari imetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakuu wa mikoa Tanzania juu ya umuhimu wa matumizi na faida ya utumiaji wa anuani za makazi nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Akifungua mafunzo hayo leo tarehe 13 Novemba, 2021 jijini Dodoma, Waziri wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Ashatu Kijaji ameagiza wakuu wote wa mikoa ya Tanzania bara kuhakikisha wanahamasisha umuhimu wa anuani ya makazi.
Aidha, Dk. Kijaji amewaagiza wakuu hao wa mikoa kuhamasisha wadau juu ya umuhimu wa mfumo wa matumizi ya utumiaji wa anuani za makazi nchini.
Pia amewataka kuelekeza na kusimamia mchakato sahihi kwa kutambua maeneo ya vijijini na miji kwa kuyapatia majina kwa lengo la urahisi wa kufanya utambuzi.
“Tuhamasisha halmashauri zote kutunga na kupitisha sheria ndogo kwa umuhimu wa kusimamia vyema mfumo mzima wa anuani za makazi,” amesema.
“Iwapo mfumo wa utumiaji wa anuani za makazi utakamilika na kutumika vizuri utachangia kasi kikubwa katika masuala ya maendeleo,” amesema.
Amesema mfumo huo wa anuani za makazi utakapokuwa umekamilika na kutumiwa vizuri upunguza muda wa kufuata bidhaa mbalimbali.
“Kila mmoja anajua kuwepo kwa janga kubwa la ugonjwa wa Uviko-19 la tumekuwa katika muyumbo wa wa uchumi na kusababisha zaidi kufanya kazi kwa njia mtandao” amesema Dk. Kijaju.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara husika Dk. Zainabu Chaula amesema iwapo wakuu wa mikoa wakielewa vizuri na kuhamasisha halmashauri ni wazi kuwa gharama za maisha zitapungua na bidhaa zitakuwa zinamfikia mteja kwa wakati.
Akizunguzia ushiriki wa umuhimu wa anuani za Makazi, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (Elimu), Gelard Mweli amesema Tamisemi imekuwa ikiandaa miundombinu rafiki ya kumfikia mwananchi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uendelezaji wa anuani za makazi.
Aidha amesema kwa sasa kumekuwepo na juhudi za kuunda kamati mbalimbali za mitaa kwa lengo ya kuboresha mfumo huo.
Leave a comment