Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi yazungumzia ofisi za Chadema kuchomwa moto
Habari za Siasa

Polisi yazungumzia ofisi za Chadema kuchomwa moto

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe nchini Tanzania, limesema linafanya uchunguzi wa tukio la ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Tunduma kuchomwa moto na watu wasiojuliakana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Ofisi hizo zimetekelea usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Oktoba 2021.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Songwe, Janeth Magomi, baada ya uongozi wa Chadema Jimbo la Tunduma, kufikisha taarifa za tukio hilo ofisini kwake ukitaka uchunguzi ufanyike ili kubaini wahusika.

“Sasa hivi tuko kwenye upelelezi, tunaomba mwananchi mwenye taarifa aje ashirikiane na Polisi wakati na sisi tunaendelea kutafuta taarifa za kiinteljensia kufahamu nani alifanya tukio lile,” amesema Kamanda Janeth

Kamanda Janeth amekemea vitendo hivyo vya uchomaji moto ofisi za vyama akionya atawachukulia hatua watakaobainika kuhusika navyo.

“Jeshi la Polisi Songwe, tunalikemea hili sio tukio zuri, ni tukio baya hasa ikiendelea kila ofisi za chama zikiendelea kuchomwa moto tutaifikisha nchi wapi? Sisi tunalikemea vikali na lisirudie tena wakati huo tunaendelea kufuatilia ambao walihusika kuchoma moto,” amesema Kamanda Janeth

Kamanda huyo amesema uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi Songwe, umebaini kuwa wahalifu hao walivunja mlango na kuchoma nyaraka zilizokuwa katika ofisi hiyo.

“Tumefika eneo la tukio na kukuta kilichochomwa ni nyaraka za ofisi na mbinu iliyotumika kuvunja mlango kwenda direct kwenye nyaraka kuchoma moto. Pale nje mlangoni tuliona nguo ambazo nazo zilichomwa moto, tulichoona mlango umevunjwa, viti, meza havijaungua. Palipoungua ni karibu na dirisha ambako kulikuwa na nyaraka mbalimbali,” amesema.

Mapema leo, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa, aliliomba Jeshi la Polisi liwachukulie hatua watu waliohusika katika tukio la kuchoma ofisi hizo.

“Tunatoa wito wa Jeshi la Polisi kutoogopa kuwachukulia hatua hawa wahalifu wanapobainika hata kama wanatoka Chama cha Mapinduzi wakidhani nafasi zao Jeshini zitakua hatiani,” amesema Mchungaji Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!