Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Temeke kuanzisha gulio, NMB kuwafunda machinga na wajasiriamali
Habari za Siasa

Temeke kuanzisha gulio, NMB kuwafunda machinga na wajasiriamali

Spread the love

 

BENKI ya NMB nchini Tanzania, imesema katika kufanikisha Kampeni ya Temeke Gulio inafanikiwa, watatoa mafunzo na mikopo kwa wamachinga na wajariamali wa wilaya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa jana Jumatano tarehe 13 Oktoba 2021 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard wakati akizungumza katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo na waandishi wa habari.

Richard alisema benki hiyo ni benki namba moja nchini hivyo imeamua kuungana na mkuu wa wilaya kutoa elimu kwa Machinga na wajasiriamali wilaya humo.

“NMB tunashirikiana na Manispaa ya Temeke katika utekelezaji wa Kampeni ya Temeke Gulio ambapo sisi tutaoa elimu na mikopo nafuu kwa wajasiriamali na wamachinga watakao kuwa tayari,” alisema.

Alisema wanaamini makundi hayo yakipata elimu sahihi kuhusu ujasiriamali na mikopo wataweza kushiriki kukopa ili kukuza biashara zao.

Meneja huyo alisema NMB inatoa mikopo ya fanikiwa inayoanzia Sh.500,000 hadi Sh.5 milioni, SME Sh.5 milioni hadi Sh.50 milioni, mikopo ya bodaboda na bajaji.

“NMB imetenga Sh.100 bilioni kwa ajili ya kukopesha wakulima, wavuvi na wafugaji nchi nzima kwa asilimia 10 tu,” alisema.

Alisema pamoja na elimu ya masuala ya fedha, wajasiliamali pia watapata fursa ya kufunguliwa akaunti zinazoendana na biashara zao kama vile fanikiwa akaunti wekeza akaunt na akaunti za muda maalumu.

Halikadhalika, Richard alisema pia wanatoa bima za magari, nyumba na vitu mbalimbali.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameipongeza benki ya NMB kwa kuamua kushirikiana na wilaya hiyo kuhakikisha kampeni ya Temeke Gulio inafanikiwa.

Jokate alisema anaamini kupitia mafunzo na mikopo ambayo itatolewa na NMB ni wazi Temeke itakuwa imekuza uchumi kwa watu wake.

Kwa upande mwingine, DC Jokate alisema pamoja na NMB pia kampuni ya Cocacola na inayozalisha mafuta, mchele na tambi za Korie wameshiriki kwenye kampeni hiyo.

Kampeni ya Temeke Gulio itashirikisha maeneo 20 ya wilaya ya Temeke ikiwemo masoko ambayo yalijengwa na Mradi wa Kuendeleza Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Mkuu huyo wa wilaya alisema, Temeke Gulioni ni fursa kwa wafanyabiashara hususan machinga kutangaza biashara zao na wao kama viongozi kuwaunganisha na fursa mbalimbali za kibiashara na itakapokuwa tayari watawajulisha.

“Dar es Salaam ni jiji la biashara, sasa lazima tuonesha biashara mbalimbali na sisi Temeke tunaanza na Temeke Gulioni. Tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutuunga mkono,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!