Tuesday , 30 April 2024
Home Kitengo Michezo Onyango, Kanoute ‘out’ dhdi ya Biashara Leo
Michezo

Onyango, Kanoute ‘out’ dhdi ya Biashara Leo

Spread the love

 

Beki wa kati wa klabu ya Simba Josh Onyango pamoja na kiungo wa mkabaji Sadio Kanoute wataukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United mara baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga.  Anaripoti Mintanga Hunda TUDARCo…(endelea)

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii ulipigwa Jumamosi ya Septemba 25, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na Yanga kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii uliashilia ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22, ambapo leo Simba itashuka dimbani majira ya saa 10 jioni kuwakabili Biashara United kwenye Uwanja wa Karume Mkoani Mara.

Thadeo Lwanga, kiungo wa klabu ya Simba

Katika kikosi kilichosafiri kwenda mkoani humo, klabu ya Simba ilitoa taarifa ya kutokuwepo kwa nyota hao wawili kwenye mchezo wa leo mara baada ya kubakia Dar es Salaam kwa matibabu Zaidi.

Wawili hao wataungana na Thadeo Lwanga ambaye ataukosa mchezo wa leo kufuatiwa kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita wac Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na hivyo atakaa nje kwa michezo miwili.

Josh Onyango, Beki wa Simba

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wataanza mbio ya kulitetea taji hilo, mara baada ya kulichukua katika kipindi cha miaka minne mfululizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!