Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Kesi ya Mbowe: Mshtakiwa adai hakupewa chakula kwa siku 10
Tangulizi

Kesi ya Mbowe: Mshtakiwa adai hakupewa chakula kwa siku 10

Spread the love

 

MOHAMMED Ling’wenya, mshtakiwa wa tatu katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake amedai, alikaa mahabusu kwa siku 10 pasina kupewa chakula chochote. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ling’wenya ametoa madai hayo leo Jumanne, tarehe 28 Septemba 2021, mbele ya Jaji Mustapha Siyani, wakati akiongozwa na wakali Peter Kibatala kutoa ushahidi wake katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Akijibu swali aliloulizwa na Kibatala aliyetaka kujua hakula kwa siku ngapi, Ling’wenya amedai kwa siku 10, kuanzia tarehe 9 hadi 19 Agosti 2020.

Ling’wenya amedai kuwa, alipatiwa chakula alivyofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Wakili Kibatala alimuuliza ilikuwaje hakula katika kipindi hicho, mshtakiwa huyo amejibu akidai walikuwa wanahudumiwa mahabusu wengine.

Amedai kilichomsaidia, katika chumba cha mahabusu alichokuwa yeye peke yake, kulikuwa na bomba la maji ndilo lilimsaidia kuwa anayatumia na wakati wote akiwa mahabusu amedai alikuwa amefungwa pingu.

Ling’wenya anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo katika kesi hiyo ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili, Adam Kasekwa, yasitumike kama ushahidi wa jamhuri mahakamani hapo kwa madai yalichukuliwa kinyume cha sheria.

Ling’wenya na Kasekwa walikamatwa maeneo ya Rau, Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 5 Agosti 2020, kwa kosa la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, watuhumiwa hao baada ya kukamatwa Kilimanjaro, walifikishwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, kisha kuhamishiwa Kituo cha Polisi Mbweni.

Hata hivyo, washtakiwa hao wawili wakitoa ushahidi wao kwa nyakati tofauti, wamedai hawakufikishwa kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam bali walipelekwa kituo cha polisi Tazara na baadaye kuhamishiwa kituo cha polisi Mbweni.

Shahidi huyo anaendelea kutoa ushahidi wake…

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

error: Content is protected !!