Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hukumu ya Sabaya, wenzake Oktoba mosi
Habari za SiasaTangulizi

Hukumu ya Sabaya, wenzake Oktoba mosi

Lengai Ole Sabaya akiwa mahakamani Arusha
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga tarehe 1 Oktoba 2021, kutoa hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Na. 105/2021, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Tarehe hiyo imepangwa leo Jumanne, tarehe 24 Agosti 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza ushahidi.

Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine ni, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, ambao wanadaiwa kuvamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya Sh. 2.7 milioni, katika duka la Mohamed Saad, tarehe 9 Februari 2021.

Shahidi wa mwisho upande wa utetezi, ambaye alitoa ushahidi wake leo, alikuwa ni Mbura, akiongozwa na jopo la mawakili wa utetezi, likiongozwa na Wakili Dancan Oola.

Baada ya ushahidi huo kufungwa, Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, aliiomba mahakama hiyo itoe siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho ya kesi hiyo kwa njia ya maandishi.

Hakimu Amworo alikubali ombi hilo na kutoa siku saba kwa pande zote mbili, kuwasilisha majumuisho hayo.

Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili Kweka amesema wanasubiri muda wa kuwasilisha majumuisho hayo.

“Mashahidi kama mlivyoona walikuwa 11, tulikuwa na vielelezo nane, ambavyo vyote vilikuwa mahakamani, tumesikiliza na kupitia changamoto za kisheria toka pande zote mbili,” amesema Wakili Kweka na kuongeza:

“Tunachosubiri ni kuwasilisha majumuisho kwa pande zote, kama ilivyoelekeza mahakama. Tunasubiri hukumu, kama tulivyoelezwa na mahakama itakuwa tarehe 1 Oktoba 2021.”

Naye Wakili upande wa utetezi, Oola, amsema kesi hiyo iliyosikilizwa mfululizo kuanzia tarehe 19 Julai hadi 24 Agosti 2021, imekwenda vizuri na kwamba wanasubiri kuwasilisha majumuisho yao kwa ajili ya kuishawishi mahakama hiyo itoe hukumu ya aina gani.

“Kesi imekwenda vizuri, ilikuwa kesi ndefu yenye changamoto nyingi ila ni kawaida kwa kesi. Kinachofuata tunaenda kuandika mawasilisho ambapo tumepewa wiki moja kwa kila upande tuweze kuleta, kujaribu kuishawishi mahakama hukumu inatakiwa kuwa ya namna gani,” amesema Wakili Oola.

Sabaya na wenzake, walisomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo mhakamani hapo, tarehe 16 Julai 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!