Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ashiriki mkutano wa SADC Msumbiji
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ashiriki mkutano wa SADC Msumbiji

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameshiriki mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Msumbiji … (endelea).

Mkutano huo, umefanyika leo Jumatano, tarehe 23 Juni 2021, Maputo nchini Msumbiji.

Katika mkutano huo, umeongozwa na Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi.

Mkutano huo, ajenda mbalimbali zikiwemo zinazohusu mtangamano wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, fursa mbalimbali za kiuchumi, pamoja na changamoto za kiusalama.

Rais Nyusi amesema, jitihada za pamoja kutoka nchi wanachama wa ukanda wa SADC zinahitajika zaidi katika kukabiliana na tatizo la ugaidi linaloikabili nchi hiyo, kwani limekuwa likirudisha nyuma juhudi za maendeleo kwa Msumbiji na nchi wanachama.

SADC

Aidha, masuala mengine yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa dharura ni maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (UVIKO 19), uanzishwaji wa kituo cha majanga, masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, biashara na Uwekezaji katika ukanda wa Jumuiya hiyo ya SADC.

Rais Nyusi amezisisitiza nchi wanachama kuendelea kuunga mkono jitihada za taasisi za utafiti katika kufuatilia taarifa za kusambaa kwa UVIKO 19 na mawimbi mapya ya ugonjwa huo na kuendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia maambukizi mapya.

Kuhusu changamoto za tabianchi, Rais Nyusi amesema baadhi ya nchi wanachama zimekumbwa na uhaba wa mvua na nyingine kupata mvua nyingi zaidi na kufanya uwepo wa uwezekano kwa baadhi ya nchi kukumbwa na uhaba wa chakula.

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maenendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), umefanyika sambambana na maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo, ikiwa na kauli mbiu “ Kuimarisha Amani na Usalama, Kuhamasisha Maendeleo na Ustahamilivu wa Changamoto Zinazoikabili Dunia.”

Rais Samia amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Msumbiji na kurejea Jijini Dodoma nchini Tanzania.

1 Comment

  • Hizo barakoa wanazovaa isiwe wakitoka nje tu. Na huku nyumbani nako waendelee kuzivaa. Tuwe wakweli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!