Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lambana Dk. Mwigulu ‘msala’ wa ATCL
Habari za Siasa

Bunge lambana Dk. Mwigulu ‘msala’ wa ATCL

Spread the love

 

DAKTARI Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, ameshindwa kutoa malelezo kuhusu namna ya kulitoa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) shimoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma  … (endelea).

Hayo yamejiri wakati Dk. Mwingulu kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha ya 2021/22 leo Jumatano, tarehe 23 Juni 2021 jijini Dodoma.

Mussa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa Bunge alihoji, kwanini mpango wa kuboresha utendaji wa ATCL haujaingizwa kwenye muswada huo?

Zungu alihoji baada ya kubaini mabadiliko ya sheria ya kuliboresha shirika hilo, hayamo katika muswada huo uliobeba mapendekezo ya marekebisho ya sheria 22.

Akijibu swali hilo, Dk. Mwigulu amesema, serikali italifanyia kazi suala hilo.

“Mwenyekiti nilipokea hilo suala, sababu mjadala unaendelea ili tuweze kushirikiana Serikali pamoja na kamati, tutakapokuwa tunajibu hoja tutalizungumzia hilo suala,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Hata hivyo, Zungu amesema, kitendo hicho kinakwenda kinyume na kauli iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia mhimili huo tarehe 22 Aprili 2021, alipoagiza iwekwe mikakati ya kuboresha utendaji wa ATCL.

“Waziri Mwigulu, alipokuja Rais Samia kuhutubia Bunge alizungumzia namna ya kuilea ATCL na kuondoa tozo ambazo ATCL zinalipa, sasa humu hamna,” amesema Zungu.

Zungu amesema, alitarajia kuona serikali inapeleka bungeni mapendekezo ya sheria ya kuiondolea kodi ATCL, ikiwemo ushuru wa ndani na ada ya ndege kutua.

Bunge la Tanzania

“Maana yake waziri, national carrier (wabebaji wa kitaifa) zote duniani hazilipi local taxes (ushuru wa ndani), landing fees (ada ya kutua). Zote wanalipa ATCL na wanapata matatizo,” amesema Zungu.

Akihutubia Bunge mara ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, Samia alisema Serikali yake itaangalia namna ya kulilea shirika hilo kimkakati, ili liweze kujiendesha kwa ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!