May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Bunge la Uganda kufungwa

Spread the love

 

KUANZIA Jumatatu, tarehe 28 Juni hadi 11 Julai 2021, Bunge la Uganda litasitisha shughuli yake kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Hatua hiyo itafuatana na kusafisha majengo ya Bunge hilo baada ya maofisa wake kadhaa kubainika kuambukizwa virusi hivyo.

Mkurugenzi wa mawasilianona masuala ya umma katika Bunge hilo, Chris Obore amesema, uamuzi huo umechukuliwa ili kuzuia jengo hilo kuwa kitovu cha maambukizi.

Amesema, ni kutokana na idadi kubwa ya watu na maofisa kutembelea bunge hilo mara kwa mara.

Bunge la sasa la Uganda lina jumla ya wabunge 529, ikiwa ni nje ya wahudumu wa Bunge, maafisa wa usalama, waandishi wa habari na watoaji wa huduma mbalimbali.

Tangu mwezi Mei, Bunge limekuwa na matukio muhimu ikiwa ni pamoja na kusomwa bajeti na Hotuba ya hali ya taifa ambayo hutolewa na rais.

Mamia ambao walihudhuria matukio hayo, walitakiwa kufanya vipimo vya corona na waliopatikana na maambukizi, walitakiwa kujitenga.

Taarifa zaidi zinaeleza, wabunge 10 na maofisa wanne wa Bunge walikutwa na maambukizi ya virusi.

error: Content is protected !!