HASHIMU Rungwe, aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania, kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) mwaka 2020, ameshauri Rais Samia Suluhu Hassan aifanyie kazi sera yake ya kugawa chakula bure kwa wananchi (ubwabwa).
Rungwe ametaja maeneo muhimu ya utekelezwaji wa sera hiyo aliyoinadi wakati wa kampeni za uchaguzi huo, ni shuleni na hospitalini.
Mwanasiasa huyo ametoa ombi hilo leo Jumatano, tarehe 23 Juni 2021, alipozungumza na MwanaHALISI Online, ofisi kwake Makumbusho, Dar es Salaam.
Amemshauri Rasi Samia aandae mkakati utakaowezesha ajenda hiyo kutekelezwa, ili kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na njaa shuleni na wagonjwa wanaolazwa hospitali.
“Serikali ipange mpango wa kutoa bure chakula hospitalini kwa wagonjwa wanaolazwa na wanafunzi wapate mlo wa chakula. Sio wang’anganie kusoma wakiwa na njaa, wahakikishe wanafunzi wanaokwenda shule, wanapata chakula kama inavyofanywa na shule binafsi,” amesema Rungwe.
Katika kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa 2020, Rungwe alijizolea umaarufu kwa sera yake ya kugawa ‘ubwabwa’ bure shuleni na hospitalini.
Katika kampeni hizo, Rungwe alisema serikali yake itatenga fedha kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Leave a comment