Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kherry James atoa ahidi nzito
Habari MchanganyikoTangulizi

Kherry James atoa ahidi nzito

Kheri James, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
Spread the love

 

SIKU mbili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, Kherry James amesema ‘sintokuwa mtawala bali mtumishi wa wananchi.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kherry ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021, baada ya Amosi Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kumwapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Ubungo.

Kiongozi huyo kijana, amesema uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwao unalenga kuwa watetezi wa wananchi na kuwapa unafuu.

“Tutajipa dhamira yake kututeua kwa  kuhakikisha uteuzi wetu unawapa nafuu wananchi,  ambao tunaenda kuwatumikia na tuwahakikishie wananchi wa wilaya zetu kwamba,  hatuji kuwa watawala bali tunakuja kuwa watumishi wenu katika kazi ya ukuu wa wilaya,” amesema Kherry.

Almas Nyangassa, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla

Kherry ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), amewaomba wananchi wa Ubungo kumpa ushirikiano katika utekezaji wa majukumu yake mapya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!