SIKU mbili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, Kherry James amesema ‘sintokuwa mtawala bali mtumishi wa wananchi.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Kherry ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021, baada ya Amosi Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kumwapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Ubungo.
Kiongozi huyo kijana, amesema uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwao unalenga kuwa watetezi wa wananchi na kuwapa unafuu.
“Tutajipa dhamira yake kututeua kwa kuhakikisha uteuzi wetu unawapa nafuu wananchi, ambao tunaenda kuwatumikia na tuwahakikishie wananchi wa wilaya zetu kwamba, hatuji kuwa watawala bali tunakuja kuwa watumishi wenu katika kazi ya ukuu wa wilaya,” amesema Kherry.
Kherry ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), amewaomba wananchi wa Ubungo kumpa ushirikiano katika utekezaji wa majukumu yake mapya.
Leave a comment