Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM, waziri wavutana bungeni, kisa ‘tuition’
Habari za Siasa

Mbunge CCM, waziri wavutana bungeni, kisa ‘tuition’

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

 

MBUNGE wa Bukoba Vijijini mkoani Kagera (CCM), Jason Rweikiza, amevutana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kuhusu zuio la michango ya wazazi katika kugharamia masomo ya ziada (tuition.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mvutano huo umeibuka leo Jumatatu, tarehe 21 Juni 2021, katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya serikali, kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, baada ya Rweikiza kusema, katazo hilo linauwa maendeleo ya elimu nchini.

“Watoto wanajitolea kusoma, wazazi wanajitolea kuchanga chochote kitu, mtu mmoja anakaa wizarani anatoa waraka, inashangaza kweli.  Kwa nini anazuia, inamhusu nini yeye? Kuna mtu mmoja alisema, ukitaka kuuwa Taifa, uwa elimu,” amesema Rweikiza.

Baada ya Rweikiza kutoa malalamiko hayo, Prof. Ndalichako aliomba kutoa taarifa na kumueleza mbunge huyo kuwa, Serikali imekataza utaratibu huo, kwa kuwa unakwenda kinyume na Sera ya Serikali ya utoaji elimu bila malipo.

Waziri huyo wa elimu alisema, Serikali imezuia masomo ya ziada katika shule ambazo zinawalazimisha wazazi kutoa michango hiyo.

“Nimpe taarifa kwamba, shule ambazo sisi tumezuia,  ni zile wanalazimisha wazazi kuchanga hela.  Kwa hiyo suala la kwamba watu wanajitolea sio kweli,  wanalazimishwa  kinyume na maelekezo ya Serikali ya elimu bila malipo,” amesema Prof. Ndalichako.

Hata hivyo, Rweikiza alikataa kupokea taarifa hiyo, akisema zuio hilo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu ya watoto, kwa kuwa wengi wanafeli katika mitihani ya Taifa, kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwemo uhaba wa walimu.

“Ninachosema ni kwamba, nchi hii inatumia utaratibu wa mitihani.  Mtoto akifeli ameishia hapo,  ndiyo mwisho wa elimu yao, wazazi na walimu wanajitoela kusoma hakuna anayelazimisha mchango. Serikali inaharibu elimu, wizara ya elimu ina haribu elimu, taarifa hiyo siikubali naikataa,” amesema Rweikiza.

Mbunge huyo wa Bukoba Vijijini amesema, katika kipindi cha likizo, wazazi na walezi wa wanafunzi walioko katika maandalizi ya mitihani ya Taifa, hasa ya kumaliza elimu ya sekondari, hutoa michango kwa ajili ya watoto wao wapate masomo ya ziada.

“Lengo la kufanya kambi tangu enzi hizo na yeye ni Profesa anajua,  asingefikia hapo bila kufanya hivyo. Amesoma kwa bidii ya wazazi,  kwa nini anazuia utaratibu huu? Mimi nasema ni mzuri, kule mjini hawalipi fedha kwa kulazimishwa, wanalipa fedha ndogo ndogo  sababu ya kupenda na ndiyo walioomba,” amesema Rweikiza.

Rweikiza amesema, wanafunzi wengi hufeli mitihani kwa kuwa wanakosa maandalizi ya kutosha, kutokana na uhaba wa walimu nchini.

“Elimu yetu bado ya mitihani, mtoto akitaka kusonga mbele lazima afaulu mitihani,  aende hatua nyingine mpaka vyuoni  aweze kuhitimu, akifeli mitihani hawezi kwenda huko. Wafaunzi kidato cha nne wanajisomea kwa mpango wa kufaulu,” amesema Rweikiza na kuongeza:

“Na wanafunzi wana shida nyingi, mtoto anaweza akawa anaumwa hajenda shule, uwezo wa wazazi mdogo wana amua kubaki kujisomea. Au walimu hawatoshi , walimu wanaamua kujitolea muda wa ziada,  watoe elimu  ambayo wanafunzi wameikosa nyuma.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!