Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kisa mavazi: Ndugai amtimua mbunge bungeni, atoa maagizo
Habari za Siasa

Kisa mavazi: Ndugai amtimua mbunge bungeni, atoa maagizo

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ametoa maagizo kwa walinzi wa Bunge hilo, kutowaruhusu wabunge wanaovaa vibaya kuingia bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ni baada ya leo Jumanne, tarehe 1 Juni 2021, kumtoa ndani ya ukumbi wa Bunge, mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichwale, kutokana na kuvaa mavazi yasiyo ya kibunge.

Ilikuwa baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, akasimama mbunge wa Nyang’wale (CCM), Hussein Amar kuomba mwongozo.

“Spika nasimama kwa kanuni ya 170 inayohusu mavazi ya staha kwa wabunge, kanuni imeeleza wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha,” amesema Amar.

Mbunge wa Nyang’wale (CCM), Hussein Amar

 

Baada ya kutoa mwongozo huo, Spika Ndugai alimwomba atoe mfano wa mbunge ambaye hajavaa vizuri.

Mbunge huyo alisimama na kusema “mbunge huyo yuko hapo katika mkono wangu wa kulia, amevalia tisheti lakini naomba umuite mbele hapo uone suruali aliyovaa namna ilivyobana, amevaa miwani.”

Mara baada ya kumaliza kumtaja, Spika Ndugai alisimama na kumtaka mbunge huyo asimame na aondoke ndani ya ukumbi ili akavae mavazi yenye staha.

Spika Ndugai ameagiza askari wote katika milango ya kuingia bungeni wawe makini wasiruhusu wabunge kuingia wakiwa wamevaa mavazi yaliyokatazwa.

1 Comment

  • Ni kweli nguo alizovaa hazina staha? Spika unaishi nchi gani na karne gani? Hiyo nguo ni ya kawaida kabisa wala haina dosari. Mumehudhuria gwaride la majeshi na mumeona askari wetu wa kike wanavyovaa suruali wakati wakipita mbele ya Rais?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!