May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Greenwood aondolewa kikosini England Euro

Spread the love

 

KLABU ya Manchester United imethibitisha kuondolewa kikosini kwa kinda wake Mason Greenwood mara baada ya kupata majeraha katika kuelekea fainali ya michuano ya Euro itakayoanza juni 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kinda huyo alijumishwa kwenye kikosi cha wachezaji 33 wa awali ambao waliitwa na kocha mkuu wa timu hiyo Gareth Southgate kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Manchester United ilieleza kuwa kinda huyo mwenye miaka 19, atasalia kwa ajili ya matibabu Zaidi kujiandaa na msimu ujao wa Ligi.

Southgate kocha wa timu ya Taifa ya England

Aidha klabu hiyo iliendelea kusema kuwa majeruhi aliyoyapata mchezaji huyo ndio yaliyomuweka nje kwenye kikosi cha England kilichoshiriki michuano ya Euro kwa vijana chini ya umri wa miaka 21.

Pia kwa upande mwengine Southgate atataweka wazi majina 26 ya wachezaji wa timu ya Taifa ya England watakaokwenda kwenye michuano hiyo baadae hii leo.

Mchezaji huyo alikuwa tegemeo ndani ya klabu yake kwenye msimu ulioisha mara baada ya kucheza michezo 31 na kufunga mabao saba.

error: Content is protected !!