Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awang’oa mabosi Takukuru, Bunge
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awang’oa mabosi Takukuru, Bunge

Nenelwa Mwihambi, Katibu wa Bunge la Tanzania. 
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Bunge la Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Mabadiliko hayo, yametangazwa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, leo Jumamosi, tarehe 15 Mei 2021.

Katika mabadiliko hayo, Rais Samia amemtea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Rashid Hamduni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa (Takukuru).

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Rashid Hamduni

Hamduni, anachukua nafasi ya Brigegia Jenerali John Mbungo ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Pia, Hamduni amempandisha kuwa Kamishna wa Polisi (CP).

Brigedia Jenerali, John Mbungo

Katika mabadiliko mengine ambayo ameyafanya Rais Samia ni kumteua Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Tanzania.

Nenelwa Mwihambi, Katibu wa Bunge la Tanzania.

Mwihambi alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge-Ofisi ya Bunge, anachukua nafasi ya Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Kagaigai amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu tarehe 7 Oktoba 2017, alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, kushika wadhifa huo, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Dk. Thomas Kashillila, ambaye wakati huo, ilielezwa atapangiwa kazi nyingine.

Steven Kigaigai, aliyekuwa Katibu wa Bunge

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge, Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!