July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia ateua mrithi wa DPP Biswalo

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Sylvester Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kabla ya uteuzi huu, Mwakitalu, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, anachukua nafasi ya iliyoachwa wazi na Biswalo Mganga ambaye tarehe 11 Mei 2021, aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Pia, Rais Samia amemteua Joseph Pande kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (DDPP). Pande anachukua nafasi ya Edson Athanas Makallo ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP), Biswalo Mganga

Uteuzi huu, umetangazwa leo Jumamosi, tarehe 15 Mei 2021 na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Msigwa amesema, wateuliwa hao, wataapishwa Jumanne, tarehe 18 Mei, 2021 kuanzia saa 9:00 alasiri, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!