RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Bunge la Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Mabadiliko hayo, yametangazwa na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, leo Jumamosi, tarehe 15 Mei 2021.
Katika mabadiliko hayo, Rais Samia amemtea Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Rashid Hamduni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa (Takukuru).

Hamduni, anachukua nafasi ya Brigegia Jenerali John Mbungo ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Pia, Hamduni amempandisha kuwa Kamishna wa Polisi (CP).

Katika mabadiliko mengine ambayo ameyafanya Rais Samia ni kumteua Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Tanzania.

Mwihambi alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge-Ofisi ya Bunge, anachukua nafasi ya Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kagaigai amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu tarehe 7 Oktoba 2017, alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, kushika wadhifa huo, akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Dk. Thomas Kashillila, ambaye wakati huo, ilielezwa atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Bunge, Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Leave a comment