Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bosi zamani TRA ateuliwa Udart
Habari Mchanganyiko

Bosi zamani TRA ateuliwa Udart

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk. Edwin Mhede kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Uteuzi wa Dk. Mhede, umetangazwa leo Jumamosi, tarehe 15 Mei 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ambaye amesema, anachukua nafasi ya John Nguya ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kutenguliwa kwa uteuzi wa Nguya, umefanyika ikiwa ni takribani wiki mbili zimepita, tangu Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka mkoani Dar es Salaam.

John Nguya

Katika ziara hiyo, Majaliwa alisema, Nguya ameshindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo na kuufanya wakala huo, kutoa huduma chini na malengo na kuahidi kufikisha suala lake kwa mamlaka ya uteuzi kwa hatua zaidi.

Dk. Mhede, aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameteuliwa ikiwa zimepita siku 41 tangu alipomwondolewa TRA na nafasi yake kuteuliwa Alphayo Kidata.

Rais Samia, alimteua Kidata kuwa Kamishna wa TRA, tarehe 4 Aprili 2021.

Dk. Mhede, aliongoza TRA kuanzia 8 Januari 2019, akichukua nafasi ya Charles Kichere ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Njombe. Kwa sasa Kichere ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Mhede alikuwa naibu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!