Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mei Mosi: Mambo 11 aliyosema Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Mei Mosi: Mambo 11 aliyosema Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, amewahutubia kwa mara ya kwanza, wafanyakazi na kutoa ahadi mbalimbali zenye kurejesha tabasamu miongoni mwao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia, amewahutubia leo Jumamosi, katika siku ya Mei Mosi 2021, iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Katika hotuba yake ya kwanza kuitoa kwa wafanyakazi, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, Rais Samia ametumia takribani dakika 35, kuzungumzia masuala mbalimbali.

Aliingia madarakani, baada ya aliyekuwa Rais, John Pombe Magufuli, kufariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam.

MwanaHALISI Online, limebainisha mambo makubwa 11, ambayo Rais Samia ameyazungumzia kwenye hotuba hiyo na yanayoendeleza mijadala sehemu mbalimbali

Mambo hayo ni;

1. Amepunguza kodi ya mshahara (Paye) kutoka asilimia tisa hadi nane
2. Kupunguza mfumo wa bei
3. Ametangaza ajira mpya 40,000
4. Watumishi 85,000 hadi 90,000 watapandishwa vyeo
5. Mabadiliko ya muundo wa utumishi
6. Kulipa malimbikizo ya mishahara
7. Kulipwa mafao ya waliostaafu, darasa la saba na waliiondokewa kazini kwa vyeti feki
8. Kufutwa tozo ya asilimia sita ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na kubaki asilimia 15
9. Umri wa mtegemezi kwa mtoto umeongezwa kutoka miaka 18 hadi 21.
10. Kuiangalia upya sheria ya bodi ya walimu
11. Ataongeza mishahara Mei Mosi ya mwaka 2022

1 Comment

  • Gharama za maisha na bei ya mahitaji zinazidi kupaa. Hivyo thamani ya mshahara anaolipwa mfanyakazi inapungua kila kukicha. Mfanyakazi anapunjika wakati mfanyabiashara ni rahisi kupandisha bei ya bidha anayouza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!