May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mei Mosi: Watumishi wote chuo cha mipango wapewa Sh.100,000

Spread the love

 

CHUO cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kimetumia Sh.29.4 milioni, kutoa motisha kwa wafanyakazi wake wote kuanzia ngazi ya chini hadi Profesa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kila mtumishi, bila kujali nafasi yake, atapewa Sh.100,000, ikiwa ni kutambua mchango wa kila mmoja, katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ‘Mei Mosi’ yam waka 2021.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi, tarehe 1 Mei 2021 na Makamu Mkuu wa chuo hicho-Taaluma, Dk. Provident Dimoso, alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari, muda mfupi baada ya kumalizika sherehe za Mei Mosi, mkoani Dodoma.

Amesema, hatua hiyo imetokana na uongozi kukubalina na kutambua, maendeleo ya chuo hicho yanatokana na ushirikiano wa viongozi na wafanyakazi wote.

Dk. Dimoso amesema, chuo kimetoa kiasi cha Sh.29.4 kwa watumishi 294, ambapo kila mmoja atapata Sh.100,000 kuanzia muhudumu wa ngazi ya chini hadi mkuu wa chuo bila kujali nafasi ya mtumishi.

Amesema, utawala wa chuo hicho, ulifikilia kutoa zawadi kwa wafanyakazi wote bila kubagua kwa kutambua, maendeleo ya chuo hicho yanatokana na umoja, upendo na mshikamano kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati.

“Zawadi hiyo ambayo imetolewa kwa siku ya Mei Mosi, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, chuo kimeona ni vyema kutoa motisha kwa wafanyakazi, kuanzia ngazi ya waendeshaji, wahudumu, wafanyausafi, walinzi, maofisa uhusiano na wahasibu wote kwa pamoja wamefanikisha kufanya chuo kuwa na maendeleo,” amesema Dk. Dimoso.

“Unaweza kuona ndani ya miaka miwili ya nyuma, chuo kilikuwa na wanafunzi 8,000 lakini kwa sasa wapo wanafunzi 15,000, miaka miwili ya nyuma, chuo kilikuwa na heka 60, lakini kwa sasa wana heka 700 ambazo chuo kimenunua kwa fedha taslimu na yapo magari mapya sita ikiwemo gari maalumu ya kuwahudumia wafanyakazi,” amesema.

Dk. Binirith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Dk. Dimoso amesema, “kwa mafanikio hayo, sehemu kubwa inatokana na ushirikiano mzuri wa watumishi, waendeshaji pamoja na watoa huduma kila mmoja kwa nafasi yake jambo ambalo linafanya utawala kuona umuhimu wa kutoa zawadi kwa wafanyakazi hususani kwa siku muhimu kama ya leo.”

Kiongozi huyo amesema, pesa iliyotolewa kwa watumishi hao imegawanywa sawa kwa sawa kuanzia mtumishi wa chini kabisa kwa profesa na fedha hiyo tayari imewekwa kwenye akaunti ya kila mmoja.

Amesema kutokana na hali hiyo, itatoa mfano bora kwa taasisi nyingine na itatoa chachu kwa wafanyakazi kwa kujituma zaidi na kwa ubora zaidi na hata wale wachache ambao walikuwa wakilegalega wataongeza juhudi zaidi na hilo ni sawa na somo jema kwao.

Awali, mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, amekemea vikali tabia za baadhi ya waajiri, kutokutoa zawadi kwa wafanyakazi kwa visingizio vya mkachato kutokukamilika na kuwapa siku mbili za kazi kukamilisha mchakato huo.

Dk. Mahenge amesema, baadhi ya waajiri wamekuwa wakionesha picha mbaya, wamekuwa wakitanguliza kutoa vyeti kwa wafanyakazi bora lakini wanapofikia suala la zawadi ya fedha wanasema mchakato haujakamilika.

“Kutokana na hali hiyo, natoa siku nne kwa halmashauri ambazo hazijatoa fedha ya zawadi kwa wafanyakazi bora, ikiwemo halmashauri ya Bahi ikamilishe mara moja” amesema Dk. Mahenge

“Ninataka hadi siku ya Jumanne tarehe 4 Mei 2021, wafanyakazi wote bora wawe wameshapata zawadi zao na nipate taarifa hiyo haraka iwezekanavyo” amesema Dk.Mahenge.

error: Content is protected !!