Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atoa ujumbe kwa Watanzania
Habari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe kwa Watanzania

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka Watazania waendeleze utamaduni wao uliodumu kwa muda mrefu wa kushikamana, kupendana na kushirikiana ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa ya amani na utulivu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Ijumaa, tarehe 2 Aprili 2021, baada ya sala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma.

Majaliwa alikuwa akiwasilisha salamu za Rais Samia kwa Watanzania.

Amesema Rais Samia anamatumaini makubwa na Watanzania wote hivyo amewataka waendelee kuwa watulivu na washiriki katika shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuboresha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

“Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, anamatumaini makubwa kwa Watanzania wote, tuendelee kuliombea Taifa letu na kila mmoja ashiriki katika shughuli za maendeleo na hatua tunayotarajia itafikishwa na sisi wenyewe na tukizingatia haya tutafanikiwa sana.”

“Serikali inaendelea na kazi na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa ofisi mpya za kudumu za wizara kwa sababu zilizopo zilikuwa za muda tu. Mkakati wa muendelezo wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu unaendelea,” amesema Majaliwa.

Amesema Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha wananchi wanaendelea kuhudumiwa na kutumikiwa huko huko walipo.

“Serikali ipo imara na imejipanga vizuri kuwahudumia na hakuna kitakachoharibika Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, yote yaliyopangwa yataendelezwa,” amesema Majaliwa

Akizungumzia kuhusu miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa nchini, Majaliwa amesema, Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia, imejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote inaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania wamuombee kwa Mwenyezi Mungu Rais pamoja na wasaidizi wake wote ili waendelee kutimiza majukumu yao ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanatimia.

“Tumeanza vizuri, tutaendelea vizuri na tutamaliza vizuri, wananchi tuendelee kumuombea rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu aendeee kuwa na afya njema ili atekeleze malengo ya kuwatumikia Watanzania na hakuna kitakachoharibika,” amesema

Kadhalika Waziri Mkuu ameedelea kuwasisitiza wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanawajengea watoto wao msingi wa kufanya ibada kwa kuongozana nao kwenye nyumba za ibada kwa kuwa dini zinanafasi kubwa ya kuwakuza katika maadili mema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!