Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maagizo ya JPM yamweka matatani Jafo, Rais Samia amtahadharisha
Habari za Siasa

Maagizo ya JPM yamweka matatani Jafo, Rais Samia amtahadharisha

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemtaka Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo kusema kama ameshindwa kudhibiti upotevu wa fedha kwenye wizara hiyo, ili apatiwe msaada. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo ya Rais Samia imetolewa leo Jumapili tarehe 28 Machi 2021, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, baada ya kiongozi huyo kukabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

“… Hangaika mara ya mwisho ukishindwa tuambie tukusaidie, lakini hali hairidhishi TAMISEMI, TAMISEMI wanachukua fedha nyingi Serikali Kuu lakini hawarudishi, naomba usimamie hilo ili fedha zinazokusanywa zisipotee na zinazokwenda zitumike zinavyostahiki,” ameagiza Rais Samia.

Rais Samia ametoa kauli hiyo akisema kwamba, Hayati Rais John Magufuli, alimpa agizo hilo Jafo zaidi ya mara mbili, lakini ameshindwa kulifanyia kazi na kusababisha upotevu wa mapato kuendelea kukithiri kwenye iwzara yake.

https://youtu.be/VLus8LdlVVc

“Kuhusu TAMISEMI, waziri uko hapa kuna upotevu mkubwa wa fedha, TAMISEMI wanafanya kama sheria zinazotungwa Serikali Kuu haziwahusu , na hili mheshimiwa Rais marehemu Magufuli alishakwambia mara mbili tatu naomba ukasimamie mapato na matumizi Tamsiemi,” amesema Rais Samia.

Dk. Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es salaam, alikokuwa anapatiw amatibabu ya mfumo wa umeme wa moyo.

Mwanasiasa huyo aliyefariki dunia akiwa madarakani, mwili wake ulizikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Dk. Magufuli alifariki dunia miezi minne, tangu alipoapishwa kumalizia uongozi wake katika Serikali ya Awamu ya Tano, tarehe 5 Novemba 2020.

Mwanasiasa huyo alianza kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano tarehe 5 Novemba 2015, baada ya kushinda kiti cha urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!