May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amuibua Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara

Spread the love

 

HATUA ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha Sh. 3.9 Bilioni, imemuibua Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rais Samia amemsimamisha kazi Mhandisi Kakoko leo Jumapili tarehe 28 Machi 2021, katika hafla ya kupokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Hatua hiyo ya Rais Samia ilichukuliwa baada ya CAG, Charles Kichere, kusema ukaguzi wake umebaini ubadhirifu TPA.

Saa kadhaa baada ya Rais Samia kumsimamisha kazi Mhandisi Kakoko, Lissu amemshauri kiongozi huyo kufanya uchunguzi wa kina katika miradi mikubwa ya maendeleo.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, ametoa ushauri huo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Lissu ameandika “Ushauri wangu, yasiishie kwa ATCL (Shirika la Ndege Tanzania) na TPA tu, uchunguzi wa kina ufanywe kwa miradi yote mikubwa ili tujuwe ukweli wake wote.”

Akiwasilisha muhtasari wa ripoti hiyo kwa Rais Samia, CAG Kichere, alisema matokeo ya ukaguzi huo yamebaini changamoto mbalimbali katika baadhi ya mashirika ya umma, ikiwemo ubadhirifu wa fedha.

CAG Kichere alidai ukaguzi wake ulibaini ubadhirifu ndani ya TPA, lakini pia ulibaini ATCL ilikuwa inajiendesha kwa hasara katika kipindi cha miaka mitano, ambapo kwa mwaka 2019/2020, ilipata hasara ya Sh. 60 Bil.

Kufuatia changamoto hizo, Rais Samia alimuagiza CAG Kichere kuyaanika mashirika yote ambayo yana viashiria vya ubadhirifu wa fedha za umma.

“Mashirika yasiyofanya vizuri CAG naomba ulimi wako usiwe na utata, kama shirika halifanyi vizuri tuambie hili halifanyi vizuri, kama bodi haifanyi vizuri sema hii haifanyi vizuri. Ukisema mapungufu tutaweza rekebisha, tukinyamazia na kutizama sura hatutasaidia wananchi,” amesema na kuongeza Rais Samia:

“Uutakaponilitea ukaguzi wa mashirika naomba uwe wazi zaidi ili tujue tunachukua hatua gani.”

error: Content is protected !!