Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC: Uchaguzi jimbo la Muhambwe Mei 2
Habari za Siasa

NEC: Uchaguzi jimbo la Muhambwe Mei 2

Spread the love

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imetangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Muhambwe, mkoani Kigoma ambao utafanyika tarehe 2 Mei 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Ni baada ya aliyekuwa mbunge wake, Atashasta Nditiye kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufariki dunia tarehe 12 Februari 2021, kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Dodoma.

NEC imetangaza uchaguzi huo, baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi.

Uchaguzi huo, umetangaza leo Jumamosi tarehe 27 Machi 2021, na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Willson Mahera, alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari.

Amesema, maandalizi kwaajili ya uchaguzi huo yameshafanyika na kazi ya utoaji fomu kwa wagombea itaanza kesho Jumapili tarehe 28 Machi hadi 3 Aprili, 2021.

Dk. Mahera amesema, uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hiyo ukifanyika 3 Aprili 2021.

Amesema kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo zitaanza 3 Aprili 2021 hadi 1 Mei na siku inayofuata ambayo ni 2 Mei 2021, ni siku ya uchaguzi huo.

Dk. Mahera amesema, tayari tume imekwisha vitaarifu vyama vya siasa kwa njia ya barua juu ya kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo na inavikumbusha kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo na maelekezo ya tume wakati wote wa kipindi cha uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!