May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbatia: Ashauri Majaliwa ajiuzulu uwaziri mkuu

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi

Spread the love

 

JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi, ametoa ushauri kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kujiuzulu ili kumfanya Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan kuunda baraza jipya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu

Mbatia amesema, hatua hiyo itamsaidia Rais Samia kuunda Serikali yake.

Ni baada ya Samia aliyekuwa makamu wa Rais, kuapishwa tarehe 19 Machi 2021, kuwa Rais, kuchukua nafasi ya Dk. John Pombe Magufuli, kufariki dunia.

Dk. Magufuli, alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021 na mwili wake kuzikwa Ijumaa ya 26 Machi 2021.

MwanaHALISI TV, limefanya mahojiano na Mbatia kuhusu mabadiliko hayo ya uongozi na jinsi anavyomfahamu Rais Samia na matarajio yake.

Kufahamu zaidi, fuatilia mahojiano yake.

error: Content is protected !!