May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto aongoza 40 ya Maalim Seif Pemba

Spread the love

 

KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amewaongoza wanachama na viongozi wa chama hicho kwenye arobaini ya Maalim Seif Sharif Hamad. Anaripoti Mwandishi Wetu…endelea.

Maalim Seif, aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais, Zanzibar alifikwa na mauti saa 5:26 asubuhi ya tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kesho yake ya tarehe 18 Machi 2021, mwili wa Maalim Seif ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, ukazikwa nyumbani kwao Nyali, Mtambwe, Pemba.

Zitto ameongoza kisomo hicho cha arobaini kimefanyika leo Jumamosi tarehe 27 Machi 2021, Kijijini Nyali Mtabwe na kuhudhuliwa na watu mbalimbali.

Baadhi ya wanachama na wasiowachama, walilazimika kuvuka vivuko kutoka katika makazi yao ili kuhudhulia arobaini hiyo ya Maalim Seif, aliyekuwa mwamba wa siasa za Zanzibar.

Kabla ya kufanyika kwa kisomo hicho cha arobaini hiyo, Zitto aliwaongoza viongozi na wanachama akiwemo makamu mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Zanzibar, Juma Duni Haji maarufu Babu Duni kwenda katika kaburi la Maalim Seif.

error: Content is protected !!