Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Kikwete aongoza maelfu ya wananchi kumuaga Maalim Seif
Habari za SiasaTangulizi

Rais Kikwete aongoza maelfu ya wananchi kumuaga Maalim Seif

Spread the love

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameongoza maelfu ya wananchi jijini Dar es Salaam, katika ibada ya swala ya maiti ya mwanasiasa mkongwe nchini, Maalim Seif Sharif Hamad. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).  

Ibada hiyo maalum kwa ajili ya marehemu, ilifanyika Msikiti wa Maamur, uliyopo eneo la Upanga, mkabala na hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Wengine waliohudhuria ibada hiyo, ni Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe.

Ibaada ya swala ya maiti ya Makamu wa Kwanza wa Rais Visiwani, iliyoanza majira ya saa 2:30 asubuhi ya 18 Februari 2021, ilimalizika saa 3 na dakika tano.

Maalim Seif (77), alifariki dunia jana Jumatano, saa 5:26 asubuhi, katika hospitali ya taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya kifo chake, ilitangazwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Katika taarifa yake kwa umma, Rais Mwinyi alisema, Maalim Seif alifikishwa katika hospitali ya Muhimbili, tokea 9 Februari mwaka huu.

Rais  Mwinyi akatangaza siku saba za maombolezo, ambapo amesema, bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Mazishi ya kiongozi huyo shupavu katika mapambano ya demokrasia nchini na Afrika, yanatarajiwa kufanyika jioni ya leo Jumatano, kijijini kwake, Mtambwe, wilaya ya Wete, mkoa wa Kaskani Pemba.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Serikali ya Zanzibar, baada ya kutoka msikitini, mwili wake uliekelea uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Unguja.

“Mara baada ya mwili kufika Unguja, utapelekwa viwanja vya Mnazi Mmoja, kwa ajili ya ibada ya swala na salam za rambirambi,” imeeleza taifa hiyo.

Aidha, mwili wa Maalim Seif utapelekwa kwenye viwanja vya Gombani, Pemba, kwa ajili ya swala, inayotarajiwa kuanza saa 7 mchana na badaye utasafirishwa hadi kijijini kwake, Mtambwe, kwa ajili ya mazishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!