May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Balozi John Kijazi afariki dunia

Balozi John Kijazi

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania, Balozi John Kijazi, amefariki dunia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea). 

Taarifa ya Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, imemnukuu Rais Magufuli akitangaza kifo hicho, kilichotokea leo Jumatano saa 3:10 usiku, tarehe 17 Februari 2021.

Msigwa amesema, taratibu za mazishi ya Balozi Kijazi zitatangazwa baadaye. Mungu amuweke mahali pema peponi, Amina.

Balozi Kijazi aliteuliwa na Rais Magufuli tarehe 6 Machi 2016 kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, akichukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue. Kesho yake yaani 7 Machi 2016 akaapishwa, kuanza majukumu hayo.

Balozi Kijazi amewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal na pia ana makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.

error: Content is protected !!