Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko BAKWATA yatoa magizo kuikabili corona
Habari MchanganyikoTangulizi

BAKWATA yatoa magizo kuikabili corona

Spread the love

 

BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limeelekeza misikiti yote kufanya maombi maalumu (kusoma dua) kwa ajili ya kumuomba Munga kuliepusha taifa na corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 14 Februari 2021, Sheikh Hassan Chizenga ambaye ni Katibu Baraza la Maulamaa amesema, misikiti yote imuelekee Mungu.

“Bakwata inatoa agizo kwa misikiti yote nchini kurejea tena kusoma kunuti (dua) katika swala zote tano hadi corona itokomee kabisa,” amesema Sheikh Chizenga.

Amesema, mwaka jana Waislam na wengine walifunga siku nne kwa ajili ya kumuomba Mungu kuwalinda, amewaomba wafanye hivyo sasa.

“Tufunge siku tatu,” amesema Sheikh Chizenga huku akisistiza, kila mmoja kufanya toba (kuomba msamaha) kwa Mwenyezi Mungu.

Soma zaidi:

Covid-19 Sheikh Ponda aungana na KKKT Katoliki

 

Pia Sheikh Chizenga ameitaka misikiti yote kurejesha utamaduni wa waumini kunawa mikono kwa maji safi na tiririka.

“Tunaitaka misikiti yote kurudisha utamadunia wa kunawa mikono kabla ya kuingia misikitini,” amesema.

Katika siku za karibuni, Bakwata inakuwa taasisi ya tatu ya dini nchini kutoa mwongozo wake kwa waumini kuhusu namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Taasisi hiyo imetanguliwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

1 Comment

  • Tunarudia kule kule tulikotoka. Kwani dua zote za mwaka jana hazikutosha?
    Sasa tunaambiwa tunawe mikono tu bila ya kuvaa barakoa na bila ya kuepuka msongamano na bila ya chanjo. Makanisa yamethubutu kwa nini Bakwata wanasita? Kama ni dua basi hata huko Saudia, Iran na Pakistan kwani wameshindwa kuomba dua? Zote hizi ni nchi za Kiislamu lakini hawategemei dua tu na kunawa mikono tu. Wanaswali na kufuata maagizo YOTE ya wataalamu
    Imefika wakati tuseme ukweli bila kufichana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!