July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BAKWATA yatoa magizo kuikabili corona

Spread the love

 

BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limeelekeza misikiti yote kufanya maombi maalumu (kusoma dua) kwa ajili ya kumuomba Munga kuliepusha taifa na corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 14 Februari 2021, Sheikh Hassan Chizenga ambaye ni Katibu Baraza la Maulamaa amesema, misikiti yote imuelekee Mungu.

“Bakwata inatoa agizo kwa misikiti yote nchini kurejea tena kusoma kunuti (dua) katika swala zote tano hadi corona itokomee kabisa,” amesema Sheikh Chizenga.

Amesema, mwaka jana Waislam na wengine walifunga siku nne kwa ajili ya kumuomba Mungu kuwalinda, amewaomba wafanye hivyo sasa.

“Tufunge siku tatu,” amesema Sheikh Chizenga huku akisistiza, kila mmoja kufanya toba (kuomba msamaha) kwa Mwenyezi Mungu.

Soma zaidi:

Covid-19 Sheikh Ponda aungana na KKKT Katoliki

 

Pia Sheikh Chizenga ameitaka misikiti yote kurejesha utamaduni wa waumini kunawa mikono kwa maji safi na tiririka.

“Tunaitaka misikiti yote kurudisha utamadunia wa kunawa mikono kabla ya kuingia misikitini,” amesema.

Katika siku za karibuni, Bakwata inakuwa taasisi ya tatu ya dini nchini kutoa mwongozo wake kwa waumini kuhusu namna ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Taasisi hiyo imetanguliwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

error: Content is protected !!