May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim Poulsen arejeshwa kuifundisha Taifa Stars

Kim Poulsen, kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Kim Poulsen raia wa Denmark (61) kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars.’ Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya Cliford Ndimbo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF aliyoitoa leo Jumatatu tarehe 15 Februari 2021 imesema, Poulsen amesaini mkataba wa miaka mitatu “kuifundisha Taifa Stars ambayo hivi sasa iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya kucheza fainali za AFCON pamoja na Kombe la Dunia ambazo zote zitafanyika mwaka 2022 nchini Cameroon na Qatar.”

Poulsen, amewahi kuifundisha Taifa Stars kati ya mwaka 2012 hadi 2013, anachukua nafasi ya Etienne Ndayiragije, rais wa Burundi, ambaye mkataba wake umesitishwa baada ya kumalizika kwa mashindo ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) yaliyofanyika Cameroon.

Baada ya kuondoka mwaka 2013, Poulsen kwa nyakati tofauti amekuwa mkufunzi wa soka la vijana kwa nyakati tofauti.

Ndayiragije aliifundisha Taifa Stars kuanzia Julai 2019 hadi Febriari 2021.

error: Content is protected !!