Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tukikukamata tutakutandika faini – DED Temeke
Habari Mchanganyiko

Tukikukamata tutakutandika faini – DED Temeke

Spread the love

 

MTU yeyote atakayekamatwa akitupa takataka katika Mamispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, atatozwa faini.Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 27 Januari 2021, na Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake.

Amewataka wakazi wa manispaa hiyo na wale wanaotumia barabara ndani ya manispaa yake, kuhakikisha wanaweka mazingira safi sambamba na utunzaji wa barabara.

“Tumetengeneza barabara za kisasa ili zichukue miaka mingi ijayo, hatutakubali Temeke kuwa eneo la kutupa takataka barabarani.

“Mtanzamia yeyote atakayepanda daladala, bodaboda, bajaji au usafiri binafsi, ukionekana umetupa takataka yoyote utakamatwa na kutandikwa faini,” amesema Mwakabibi.

Pia mkurugenzi huyo amewataka wakazi wa manispaa huyo kulipia ushuru wa takataka katika magari yanayofanya kazi ya kukusanya taka hizo.

1 Comment

  • Asante mkurugezi kwa kauli njema lakini tunakuomba utuweke sehem ya kuifadhi taka mitaani na sehem za wazi ukiwa utayatimiza hapo kweli mtupa taka ovyo anastaili kuchukuliwa hatua za kisheria

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aanika mafanikio ya TMA

Spread the loveSHUGHULI za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zimeimarika...

error: Content is protected !!