April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tukikukamata tutakutandika faini – DED Temeke

Spread the love

 

MTU yeyote atakayekamatwa akitupa takataka katika Mamispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, atatozwa faini.Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 27 Januari 2021, na Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake.

Amewataka wakazi wa manispaa hiyo na wale wanaotumia barabara ndani ya manispaa yake, kuhakikisha wanaweka mazingira safi sambamba na utunzaji wa barabara.

“Tumetengeneza barabara za kisasa ili zichukue miaka mingi ijayo, hatutakubali Temeke kuwa eneo la kutupa takataka barabarani.

“Mtanzamia yeyote atakayepanda daladala, bodaboda, bajaji au usafiri binafsi, ukionekana umetupa takataka yoyote utakamatwa na kutandikwa faini,” amesema Mwakabibi.

Pia mkurugenzi huyo amewataka wakazi wa manispaa huyo kulipia ushuru wa takataka katika magari yanayofanya kazi ya kukusanya taka hizo.

error: Content is protected !!