May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nizar Khalfan amrithi Mwambusi Yanga

Spread the love

 

NIZAR Khalfan, ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Michuano ya Mapinduzi ya Zanzibar, Yanga ya jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Nizar (32), anachukua nafasi ya Juma Mwambusi, ambaye hivi karibuni, aliiandikia barua Yanga ya kujizulu kutokana na sababu za kiafya.

Leo Jumatano, tarehe 27 Januari 2021, mitandao ya kijamii ya Yanga, imemtambulisha Nizar kwa kuweka picha yake akiwa na Mkurugenzi Mwekezaji wa kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said na Mshauri wa uongozi wa Yanga, Senzo Mazingisa.

“Karibu kwenye timu ya wananchi Nizar Khalfan, kocha msaidizi wa klabu yetu, wananchi wanategemea makubwa kutoka kwako,” wamesema Yanga

Nizar aliyezaliwa tarehe 21 Juni 1988, anakwenda kuwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi.

Kabla ya kutambulishwa na mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania, Nizar alikuwa akikinoa kikosi cha African Lyion, kinachoshiriki ligi daraja la kwanza.

Mbali na kuichezea Yanga kati ya mwaka 2012-2015, akitokea Vancouver Whitecaps ya Canada alikokipiga kuanza mwaka 2009-2011, amezichezea Mtibwa Sugar (2005-2007) na mwaka 2007 alijiunga na Al Tadhamon ya Kuwaiti kisha akatimkia Tadamon Sour Sporting ya Uarabuni na timu ya mwisho kuichezea ilikuwa Pamba ya Mwanza mwaka 2018.

error: Content is protected !!