Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo ‘wakimbilia’ kwa Biden
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo ‘wakimbilia’ kwa Biden

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, kimemsihi Joe Biden, Rais wa Marekani kupingana pia kuchukua hatua dhidi ya mataifa ya Kiafrika yanayokandamiza demokrasia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kwenye tarifa yake ya pongezi ya kuapishwa kwake (Biden), ACT-Wazalendo kimeeleza kwamba, watawala wa kiimla pamoja na wanyongaji demokrasia wanapaswa kushughulikiwa.

“Watawala wa kiimla wa Afrika wanastahili kushughulikiwa na kuwajibishwa kwa maslahi mapana ya wananchi, ili kulinda haki za wananchi za kujitawala, kulinda utawala wa sheria na haki za binadamu,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Mambo ya Nje ya chama hicho na kungeza:

“Kwa misingi hiyo basi, tuna matumaini makubwa kwamba utawala wako utafanya kazi kwa karibu na kimkakati kuhakikisha nchi za Afrika zinarejea katika kuheshimu demokrasia na utawala wa sheria hasa Tanzania.”

Taarifa hiyo imeeleza, chama hicho kiko tayari kushirikiana na Serikali ya Biden kutokana na msimamo wa rais huyo wa katika utetezi wa misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, uswa na haki za binadamu.

“Mataifa mengi ya Afrika yamerudi nyuma hatua ndefu katika kuheshimu demokrasia na utawala wa sheria. Chaguzi zimepoteza uhalali. Utawala umepoteza misingi ya uwajibikaji. udikteta na uimla umekita mizizi,” imeeleza taarifa hiyo.

Joe Biden, Rais wa Marekani

Pia imelalamikia uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, haukuwa uchaguzi, bali uhalalishaji wa chama tawala kupora madaraka ya wananchi.

“Wakati tunachukua hatua za kukupongeza kwa imani kubwa walionayo Wamarekani kwako, Chama cha ACT Wazalendo kinafungua milango kwa ajili ya ushirikiano na utawala wako.

“Chini ya Biden, tunatazamia kuiona jamii ya Marekani yenye ushamiri sambamba na kuunga mkono jitihada zetu Afrika za kuimarisha demokrasia, utawala wa sheria na ulinzi wa haki za binadamu,” imeeleza taarifa hiyo.

Biden, aliapishwa tarehe 20 Januari 2021, kuwa Rais wa 46 wa Marekani, akimpokea Donald Trump, aliyemaliza muda wake miaka minne madarakani.

2 Comments

  • Uchaguzi mkuu wa Tz haukuwa uchaguzi? Sasa mbona ACT imejiunga na chama tawala? Mbona Maalim anamwagiwa sifa kem kem na JPM?

  • Asante ndugu zitto nakupongeza kwa kushindwa kujielewa pia nakupongeza kwa kulitoa thamani bara la Africa na kuthamini bara ambalo linaidharu Africa na kumnyanyasa mtu wa Africa asante ndugu zitto endeleaza fikra potofu. Kweli sasa dunia imekueleewa ilikuwa hajakujua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!