May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Klopp: Tumepoteza mchezo ambao hatukustahili kupoteza

Jorgen Klopp, Kocha wa Liverpool

Spread the love

KICHAPO cha bao 1-0, dhidi ya Burnley, kocha kikosi cha Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa timu yake imefungwa kwenye mchezo ambao hawakustahili kufungwa huku akiongezea kuwa hauwezi kufikiria swala la ubingwa kwa sasa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Mkwaju wa penalti wa Ashley Barnes dakika ya 83, ilitosha kuifanya Burnley kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Anfield na kuvunja rekodi ya Liverpool ya kutofungwa nyumbani tangu mwaka 2017.

Baaada ya mchezo huo, kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp alisema kuwa licha ya kupoteza mchezo huo ila maamuzi ya wachezaji wake kwenye eneo la mwisho la wapinzani hayakuwa sahihi.

“Katika eneo la mwisho maamuzi yetu hayakuwa sahihi, hilo ndiyo tatizo, umepata mpira kwenye eneo sahihi badala ya kupiga shuti mchezaji anatoa pasi,” alisema Klopp na kuongeza:

“Tofauti ya mchezaji mzuri na mchezaji mzuri sana ni kwenye kufanya maamuzi uwanjani.”

Kwa matokeo haya dhidi ya Burnley yamevunja rekodi ya Liverpool ya kucheza michezo 68 ya Ligi Kuu kwenye dimba la Anfield na huku wakicheza michezo minne bila kufunga bao na mechi sita bila kupata ushindi.

Liverpool kwa sasa imeachwa nyuma kwa pointi sita na vinara wa Ligi hiyo Manchester United yenye pointi 40 na kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

error: Content is protected !!