Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ma MC, wapambaji, wamiliki wa kumbi kutozwa ada
Habari Mchanganyiko

Ma MC, wapambaji, wamiliki wa kumbi kutozwa ada

Spread the love

WATU wanaofanyakazi ya kupamba kumbi za starehe, kusherehesha (Ma-MC), wapishi wa sherehe na wapiga picha, watatakiwa kulipa ada na ushuru. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Ni baada ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza, kupitisha sheria ndogo za ada na ushuri ambazo tayari zimepata baraka za Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Barua iliyosainiwa na Emmanuel Kaponoke, Afisa Utamaduni wa halmashauri hiyo ya tarehe 15 Januari 2021 kwenda kwa walengwa, inabainisha ada hizo.

Washereheshaji (MC) watapaswa kulika Sh.50,000 kwa sherehe moja huku wapambaji kumbi za burudani/sherehe watalipa Sh.30,000.

Wamiliki wa kumbi, unaochukua watu kati ya 100-200 ni Sh.50,000 kwa siku, ukumbi unaochukua watu kati ya 201-500 atalipa Sh.100,000.

Wapishi wa vyakula kwa siku moja ya tukio atapaswa kulipa Sh.30,000 na wapiga picha za video na mnato watapaswa kulipa Sh.30,000 huku muziki ikiwa ni Sh.30,000

“Kamwe, mmiliki wa ukumbi asiruhusu sherehe kufanyika ndani ya ukumbi wake bila kibali cha halmashauri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo

“Ikumbukwe, ada hii ni kwa ajili ya kubali cha halmashauri tu na si gharama ya kukodi ukumbi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!