Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko JPM amlilia mbunge wake
Habari Mchanganyiko

JPM amlilia mbunge wake

Rais John Magufuli
Spread the love
RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa na kifo cha Martha Umbulla, mbunge wa viti maalumu kupitia ChamaCha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika salamu zake za rambirambi alizozituma kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM amesema, Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo.

“Nazikumbuka jitihada zake wakati akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,” imeeleza taarifa ya Rais Magufuli iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

Martha Jachi Umbulla

Umbulla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 21 Januari 2020, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya HCG, Mumbai nchini India.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika Ndugai akieleza “nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Mkoa wa Manyara.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!