May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Pigo CCM, mbunge wake afariki

Marehemu Martha Jachi Umbulla

Spread the love

MARTHA Jachi Umbulla, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 21 Januari 2020. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Job Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri kwamba, mbunge huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya HCG, Mumbai nchini India.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Mkoa wa Manyara.

“Mungu awape moyo wa utulivu na subra katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Ndugai na kwamba, ofisi ya bunge inaratibu mipango ya mazishi.

error: Content is protected !!