Katika salamu zake za rambirambi alizozituma kwa Job Ndugai, Spika wa Bunge, Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM amesema, Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo.
“Nazikumbuka jitihada zake wakati akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,” imeeleza taarifa ya Rais Magufuli iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

Umbulla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 21 Januari 2020, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya HCG, Mumbai nchini India.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika Ndugai akieleza “nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Mkoa wa Manyara.”
Leave a comment