May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yaivimbia Marekani 

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeitaka Marekani kueleza namna Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ulivyoingiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na gazeti moja la kila siku kuhusu kauli ya Wazir wa Mambo ya Nje ya Marekani, Michael Pompeo kuwawekea vikwazo waliohusika na kuvuruga uchaguzi huo, Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC amesema ‘hayo ni maoni yao.’

Amesema, si vema kueleza mambo kiujumla jumla na kwamba, wanapaswa kueleza ni kwa namna gani uchaguzi mkuu wa Tanzania ulivurugwa ama kuingiliwa.

Jaji Kaijage amesisitiza, uchaguzi mkuu ulihudhuriwa na waangalizi wa nje na kuwa, kama kungekuwa na tatizo lingejionesha kwenye ripoti zao.

Taarifa ya Marekani kuweka vikwanzo kwa baadhi ya maofisa wa Tanzania bila kutaja majina, iliwekwa hadharani tarehe 19 Januari 2021.

Tamko la Pempoe limelalamikia kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binadamu, wapinzani kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro, kukamatwa, kunyanyaswa na hata ufungaji wa intaneti.

error: Content is protected !!