May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TFF kuwapiga msasa viongozi klabu za Ligi Kuu

Boniface Wambura, Mkuu wa Habari na Masoko wa TFF

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuendesha Semina kwa viongozi wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ili kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya kiutawala ndani ya Tassisi hizo katika maendeleo ya mchezo huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya uwepo wa semina hiyo imetangazwa leo jijini Dar es Salaam, makao makuu ya TFF na Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Shirikisho hilo, Boniface Wambura ambae ameeleza mtililiko mzima wa semina hiyo itakavyokuwa.

Wakati akiongea na waandishi wa Habari Wambura amesema kuwa lengo la semina hizo ni kuwajengea uwezo viongozi hao huku akitaja maeneo yatakayofanyika semina hizo ambazo ni mikoa ya Morogoro, Arusha pamoja na visiwani Zanzibar.

Semina hiyo itaanza tarehe 24 Januari, 2021 kwa viongozi wa ngazi ya juu wa klabu za Ligi Kuu ambayo italenga kwenye maeneo ya utawala bora, Habari na Sheria.

“Semina hii imelenga maeneo ya utawala bora lakini pia washiriki watapata mafunzo mbalimbali kuhusu masuala yanayousiana na habari ndani ya TFF, sheria, fedha pamoja na leseni za klabu,” alisema Wambura.

Aidha Wambura aliongezea kuwa semina hiyo itaendelea siku inayofuata ya tarehe 25 Januari 2021, itafanyika visiwani Zanzibar kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) visiwani humo kwa viongozi wa klabu za huko ambao nao watapatishwa katika maeneo hayo hayo.

Pia tarehe 28 Januari 2021 itafanyika  mkoani Arusha kwa viongozi wa vyama vya soka wa mikoa ambao ni wanachama wa TFF, ili kwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa soka wa shirikisho hilo.

error: Content is protected !!