Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba ampa mtihani mzito JPM
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ampa mtihani mzito JPM

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kufuta mfumo wa vyama vingi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, chama hicho kinachoongozwa na Dk. John Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kina wabunge wengi wanaoweza kufikia theluthi mbinli na hatimaye kufanikiwa.

Ametoa kauli hiyo tarehe 20 Desemba 2020, katika kongamano la CUF la kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, lililofanyika katika Ofisi Kuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar Es Salaam.

Amesema, madhila yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu mwaka huu, yanaashiria wazi kwamba, CCM hakitaki mfumo wa vyama vingi.

“Ndugu zetu wa CCM kama hawataki mfumo wa vyama vingi, wako wengi vya kutosha ndani ya bunge. Bunge la safari hii kati ya watu 264 waliochaguliwa, wabunge wa upinzani wako nane, wao wako 256.

“Kwa hiyo theluthi mbili wanaipata Zanzibar na Bara. Kama hawana haja ya mfumo wa vyama vingi, watujulishe na wapeleke muswada ndani ya bunge walipitishe hilo,” amesema Prof. Lipumba.

Amesema, kama mfumo huo utafutwa, wapinzani watakwenda katika nyumba za ibada kumuomba Mungu.

“Kama hawana haja ya mfumo wa vyama vingi, watujulishe na wapeleke muswada ndani ya bunge walipitishe hilo, sisi twende msikiti tukaombe dua na kanisani tukafanye sala. Tushuhulikie masuala ya sala, tukamuombe Mungu,” amesema Prof.Lipumba.

Akizungumzia kongamano hilo, Prof. Lipumba amesema, chama chake kitalitumia kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanachama wake, juu ya umuhimu wa upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Rais John Magufuli

Kongamano hilo limezinduliwa rasmi takribani mwezi mmoja na nusu, tangu CUF itangaze kutoshiriki uchaguzi hadi katiba mpya na tume huru ya uchaguzi itakapopatikana.

Msimamo huo wa CUF ulitolewa na Prof. Lipumba tarehe 2 Novemba 2020, siku kadhaa baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

CUF pamoja na baadhi ya vyama vya upinzani vilitangaza kutotambua matokeo hayo yaliyokipa ushindi wa kishindo CCM, kwa madai kwamba mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, NEC ilikanusha madai hayo ikisema kwamba iliendesha mchakato wa uchaguzi huo katika misingi ya haki na usawa.

1 Comment

  • Asante ndugu lipumbumba lakini uwelewe kuwa ccm inchaguliwa na watanzania sababu ya kuichagua wanaimiin ccm na sera zake nawanamin kuwa ccm inatekereza sera zake kwa vitendo kwaio ndugu lipumbumba lawama na malalamiko yako yapeleke kwa wananchi na uwaulize kwanini mnaichagua ccm jibu lenye maana utalipata na litakusaidia ktk ulimwengu wa kisiasa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!