Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mawakili wapotoshaji kukiona – Jaji Mkuu
Habari Mchanganyiko

Mawakili wapotoshaji kukiona – Jaji Mkuu

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma
Spread the love

PROFESA Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, ameahidi kuwachukulia hatua mawakili wanaopotosha maamuzi ya mahakama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa onyo hilo leo tarehe 21 Desemba 2020, katika hafla ya uapisho wa mawakili wapya 166, iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

“Kazi ya wakili sio kupotosha maamuzi ya mahakama, kwa bahati nzuri kanuni za maadili zipo na zitatumika hata katika mitandao ya kijamii,” amesema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Juma amesema kuna baadhi ya mawakili hukiuka maadili ya taaluma zao kwa kupotosha tafsiri za amuzi wa mahakama, kupitia mitandao ya kijamii hasa twitter.

“Kuna mawakili wachache ambao bado hawaziishi kanuni za maadili, nidhamu na tabia njema inayotarajiwa kwa mawakili.

“Kila siku katika mitandao ya kijamii hasa twitter, tumeona wakitumia lugha zisizofaa,  wengine waziwazi na wengine kwa majina ya kubuni, wamejipambanua kwa kupotosha tafsiri za hukumu badala ya kuzifafanua,” amesema Prof. Juma.

Sambamba na hilo, Prof. Juma amesema, ofisi yake inapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya mawakili wasio waaminifu.

Na kwamba, kuna baadhi ya mawakili hutumia vibaya taaluma zao kuchelewesha kesi kwa makusudi ili kuwapendelea wateja wao, kinyume na sheria.

“Hata hivyo, wako mawakili wana sifa za ujanja wa kuwasaidia wateja wao kukiuka maadili kwa makusudi na kuchelewesha kesi, sidhani kati ya mawakili wapya 166 wako mawakili wa aina hiyo,” amesema na kuongeza:

“Yapo pia malalamiko yanaonesha baadhi ya mawakili kupokea malipo,  baadaye wakili huyo huona ni madogo, hayatoshi kadri kesi ilivyokuwa ikiendelea mahakamani, huanza kusumbua wateja wao na kukata mawasiliano kabisa,” amesema.

Amesema, wakati mwingine huzuia majalada na kuzuia wateja hao kutafuta mawakili wengine au kuendesha kesi wenyewe.

Kufuatia changamoto hiyo, Prof. Juma amewaasa mawakili wapya kuwa wabunifu kwa kuongeza ujuzi kuhusu taaluma yao, ili wakidhi soko la ajira.

“Kwa mujibu wa ripoti ya  Jukwaa la Uchumi Duniani la Januari 2016, lilisema utaalamu na ujuzi mbalimbali ulioko duniani pamoja na ujuzi wa sheria tunaosoma, utatoweka hivi karibuni, kwa hiyo elimu mliyoipata  inatakiwa kuendelezwa ili iweze kupambana na mazingira mapya ya ushindani wa karne ya 21,” amesema Prof. Juma.

Jaji huyo wa Tanzania amewataka mawakili wapya kujiandaa kukabiliana na changamoto ya ajira.

“Kuna jambo lingine ambalo sina budi kulizungumzia, suala la ajia katika karne ya 21, ingawa leo ni siku ya furaha, kwenu hapana shaka  haifuti wasiwasi na hofu ya mawakili wengi na wanasheria kuhusu ajira za mawakili katika ushindani wa karne hii ya 21.

“Katika hotuba yangu ya kupokea mawakili tarehe 10 Julai mwaka huu, nilizungumzia changamoto ya ajira inayowakabili mawakili wapya, nilisema siku hizi ni jambo la kawaida wanasheria wanaokubaliwa kuwa mawakili hukosa kabisa ajira katika taasisi za umma ambazo zamani zilikuwa zinaajiri asilimia kubwa ya wahitimu wa sharia,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!