Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Yanga waliamsha tena sakata la Morrison
Michezo

Yanga waliamsha tena sakata la Morrison

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela
Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela ameibuka tena na sakata la mchezaji Bernard Morrison katika kesi walizowasilisha mbele ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Hivi karibuni klabu ya Yanga ilipeleka kesi ya mchezaji huyo mbele ya TFF kuhusiana na mkataba wake aliosaini na klabu ya Simba kuwa unamapungufu na batili kisheria.

Kiongozi huyo ameongea hayo mapaema hii leo tarehe 20 Novemba, 2020, mbele ya waandishi wa Habari akisema kuwa wasiwasi wao ni endapo dirisha la usajili likifunguliwa wanaweza kubadilisha mkataba huo kwa kuwa mfumo utawaruhusu.

“Wasiwasi wetu ni kuwa tarehe 15 Decemba, 2020 dirisha la usajili linafunguliwa na huenda mkataba huo ukabadilishwa kwa kuwa mfumo utaruhusu kufanya hivyo, tunaomba TFF waitishe kesi hiyo mapema kabla ya dirisha dogo kufunguliwa.

“Kama unavyojua tuna kesi yetu CAS na mchezaji huyo na katika kijitetea Morrison aliambatanisha kielelezo cha mkataba uliosainiwa na pande zote mbili kati yake na Simba, sasa tuna wasiwasi kuwa mkataba huo uliopelekwa huko FIFA huenda ukarudishwa kwenye mfumo ikifika 15 Desemba,” aliongezea mwakalebela

Morrison alijiunga na klabu ya Simba baada ya kuwa na mgogoro wa kimkataba na Yanga na baadae kamati ya sheria, haki na hadhi za wachezaji kusema kuwa mkataba huo ulikuwa na mapungufu.

Klabu hiyo pia inataka TFF kushughulikia kwa haraka kesi waliowasilisha kwenye shirikisho hilo inayomhusu mchezaji wao Ramadhani Kabwili ya kudai kutaka kupewa rushwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!